Friday, 5 June 2009

Bongo hakuna wasomi



Bongo hakuna wasomi kama tafsiri yangu ya usomi ni mtu mwenye kuona tatizo akalitatua kwa kutumia elimu iliyojaribiwa (tried and tested). Msinishambulie kwasababu kama kungekuwa na wasomi tusingekuwa na shida ya maji wakati maji kila siku yanatiririka kwenye mito kuelekea baharini bila ya kupingwa.


Kungekuwa na wasomi wangejenga mazuio ya maji yasiende baharini ili yatumike kwa shughuli mbalimbali. na tusingepanga foleni zenye urefu wa maili kusubiri zamu ya kukinga dumu ili upate maji ya kunywa.


kama kungekuwa na wasomi barabara zetu zingetosha na foleni ya magari isingetungiwa nyimbo. na watu wasingetoa wazo la kugawa barabara moja njia tatu. mipango miji ingekuwa wazi na mamlaka husika wasingekuwa wakipata gharama za kuvunja nyumba za masikini na masikini kupata machungu zaidi maana kubomoa ni siku moja lakini kujenga ni kazi ya miaka.


kungekuwa na wasomi elimu ingekuwa ya manufaa na maisha ya wananchi yangeinuka na kupanda kiwango kila mwaka.


kungekuwa na wasomi huduma za afya zingetolewa bila rushwa na pia zingekuwa za uhakika wagonjwa wa miguu wasingepasuliwa vichwa na wagonjwa wa vichwa wasingepasuliwa miguu. ingekuwa ukifika hospitali una mategemeo ya kupona na si kumalizwa kabisa. wagonjwa wasingelazwa sakafuni, wagonjwa watatu wasingelazwa kitanda kimoja. na wodi za wagonjwa zingekuwa safi kuepusha maambukizi ya magonjwa.


kungekuwa na wasomi viwanja vya wazi visingemilikishwa kwa watu na badala yake kungekuwa na bustani na viwanja vya michezo mbalimbali. nyumba zingejengwa kiholela na kutengeza mijiovyo (slums) badala ya mipango miji safi.


kungekuwa na wasomi nisingeandika mada hii.....

Saturday, 20 December 2008

wacha tu tule pozi


Ni kawaida kwa mtu yeyote baada ya kazi ngumu au shughuli yeyote ni lazima apate angalau muda wa nusu saa au dakika 15 apumzike hii yote ni kwa ajili ya kuweka mambo sawa na kuipumzisha akili baada ya ya kufikiria kwa muda mrefu .huku matumbo yetu yakiwa yana joto kwa kusubiri matokeo ya form 4 ambayo kwa hakika siwezi kusema ni kwa nini hasa kwa nchi yetu kama hii ya tanzania mitihani inakuwa na matatizo kama yanayoendelea kujitokeza miaka hii ya karibuni.Naamini suala hili ni wazi kuwa wizara husika ndiyo ishugulikie makini

Wednesday, 28 May 2008

Vitambulisho Vya nini?


Vitambulisho vya nini katika nchi ambayo hata umeme wa uhakika bado ni changamoto. Mabilioni ya pesa ambayo yangeweza kuhakikisha shule zina vitabu vya kutosha, hospitali zina dawa za kutosha, barabara zinapitika japo kwa msimu wa kiangazi, watu wanaajira japo za kuhakikisha mlo mmoja kwa siku. Vitambulisho vya nini wakati passport zinatosha kumtambulisha mwananchi, vitambulisho vya nini wakati gharama za utengezaji ni kubwa kuliko kipato cha mlengwa. gharama za utunzaji wa kitambulisho hicho ni nani atakayelipa maana kama ni kitambulisho kilichotengezwa kwa kutumia plastiki kina "finite life time", nani atakayelipa "replacement" ya kitambulisho hicho. na kama kitakuwa na "Chip", je vifaa vya kusomea habari zilizopo kwenye hiyo chip vitawekwa kila ofisi iwe ya serikali na binafsi. kwa ufahamu wangu inabidi uwe na central database system ambayo itashughulikia uhifadhi wa habari za mwenye kitambulisho, mambo yanayohitaji kuwa na ma "computer servers " kubwa na pia watu wa kuendesha computer hizo na pia umeme wa uhakika na sio wa mgao si kwenye hizo computer farms bali na hizo "service points". faida za mradi huu kwa hakika zinashindwa na hasara zitakazopatikana, na si baada ya muda mrefu mradi utakufa na mabilioni yaliyotumika yatakuwa ni kama maji yaliyomwagika mchangani. hizo pesa zingetumika katika kutatua matatizo yanayomgusa mtanzania kila siku kama vile upatikanaji wa maji safi "on demand", upatikanaji wa huduma bora za afya na gharama nafuu, upatikanaji wa elimu bora yenye kwenda na wakati kwa gharama nafuu... VIONGOZI WETU WALIOPEWA MADARAKA YA KUFANYA MAAMUZI KWA MANUFAA YA TAIFA WANAFANYA MAAMUZI KWA MANUFAA YA KWAO WENYEWE..TATIZO TULILONALO WAAFRIKA SIO UMASIKINI WA PESA, BALI UMASIKINI WA FIKRA NA ELIMU NDIO UNAOTUANGAMIZA ZAIDI...

Monday, 11 February 2008

Tanzania Bila Rushwa Na Ufisadi Inawezekana


Kila kona ya mitaa ya Bongo utakuta bango kubwa lenye ujumbe kama linavyoonekana kwenye picha, hapo juu...ningependa kuona mabango kama hayo yenye ujumbe usemao TANZANIA BILA RUSHWA NA UFISADI INAWEZEKANA TUWEKE MIFUMO WAZI....Nimefurahi kuona wabunge wote wameungana kupigania maslahi ya wananchi badala ya kutetea maslahi ya wachache wenye tamaa zisizokuwa na mipaka katika kujikusanyia mali kwa njia zisizo halali hivyo kuhatarisha uchumi wa nchi. Muda wa kulindana umekwisha, muda wa UKADA umekwisha sasa tushirikiane wote waliopewa madaraka na wasiokuwa na madaraka, tubadili misimamo yetu kwa maslahi ya nchi kwa ujumla. ningependa kuona Rais katika baraza jipya kuna waziri japo mmoja toka katika kambi ya "UPINZANI" ili kutoa ishara kuwa michango yao katika bunge inalenga kutetea maslahi ya taifa na wananchi wake kwa ujumla, tuondokane na siasa za chuki za kuona hata kama mpinzani akileta hoja yenye kutetea wananchi basi chama tawala lazima kipinge kwa nguvu zote. Huu ni muda wa kushirikiana wote tulete maendeleo ya nchi kwa haraka..Tumechoka kuitwa nchi masikini wakati UTAJIRI wetu unachukulia hivi hivi tungali macho tena wengine tunasaidia kubeba kupeleka nje ya nchi huku wananchi wanaishi kwenye mabanda ya mabati mabovu yaliyofunikwa kwa maplastiki...

hakuna ajira vijana wamebaki kuwa wakabaji na majambazi...madada nao wamekuwa wakijiuza kwenye kwenye kona za jiji...

Wednesday, 2 January 2008

DemoCrazy Vs DemoCracy

Hivi lini Waafrika tutaamka na kuanza kuishi kama wanadamu walioendelea badala ya kubaki na fikra za kinyama, hadaa, uonevu, mauaji ya halaiki kwa tamaa za kubaki kwenye madaraka ama kutwaa madaraka bila ya idhini ya wananchi.

Waafrika baada ya kupigania uhuru toka kwa wakoloni, mababa zetu waliunda serikali chini ya chama kimoja na kuwaunganisha wananchi wote bila kujali dini, kabila na rangi zao. Japo maendeleo hayakuja kama wengi walivyotarajia na hii inatokana na ukweli kwamba nchi nyingi zilipata uhuru bila kuwa na wasomi wa kutosha wa kuendeleza rasilimali zilizoachwa na wakoloni, kwa hiyo nchi nyingi zikatumbukia kwenye dimbwi la umasikini.

Viongozi walioko madarakani wakawa wanyonyaji kwa kujinufaisha binafsi bila kujali hali halisi za wananchi wao, na hapo migogoro ikazuka na pia ukabila ukaibuka na hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe katika baadhi ya nchi. Ukitazama historia, tumekuwa watumwa, tumenyonywa, na tuaendelea kunyonywa kwasababu hatuna umoja kila mtu kivyake.

Miaka ya Tisini nchi za magharibi zikalazimisha Afrika kuwa na vyama vingi kwa jina la DEMOKRASIA, kwa mtazamo wao ilikuwa ni kutugawanya ili waweze kutunyonya zaidi kwa kufunga mikataba na yeyote atakayekuwa madarakani na kama hao walioko kwenye madaraka hawataki basi wapinzani wao watapewa misaada ili waingie kwenye madaraka hivyo kuhakikishwa kwa upande wa mataifa ya Magharibi ni 'win win situation' , kwa mtazamo wa viongozi walikuwa madarakani wakapata nafasi pia kugawanya wananchi, wenye madaraka na WAPINZANI.

Kwa mtazamo wa viongozi wa kiafrika tukapata DEMOCRAZY, wananchi wakagawika pande mbili kama mashabiki wa timu za mpira wakifuata viongozi wao bila kujali kama hao viongozi wanajali maslahi yao binafsi ama maslahi ya nchi kwa ujumla. viongozi wetu wametuingiza katika hali mbaya za kuvunjika kwa amani kwa maslahi yao binafsi nasi wananchi tunaburuzwa na kuumia, kupoteza maisha wakati viongozi wetu wakiwa katika mahekalu yao yalijaa ulinzi wakibweka amri zenye kutumaliza.

Lini tutajifunza kuwa yaliyotokea Rwanda, na Burundi yanaweza kujirudia kama mambo yalivyo Kenya hivi sasa. Wachache wenye uchu na tamaa za kubaki katika viti vya enzi kwa gharama za maisha ya wananchi wasio na hatia wataendelea kutuchimbia makaburi kabla ya muda mpaka lini. AFRIKA HAKUNA DEMOKRASIA ILA KUNA DEMOCRAZY na wanaoumia na wananchi wa kawaida.

part1....to be continued

Tuesday, 23 October 2007

Poverty in The Land of Plenty

God Blessed us with land, ever running rivers and big fresh water lakes, large reserves of minerals and vast fauna and flora and yet we are the one of the poorest nations on earth. Where have we gone wrong and why are we still doing wrong. We have huge population of which can be turned into labour force that will drive this country to prosperity.

Prosperity is everyone's dream, it is hard work if we want to prosper we need to change the way we think, act, behave, attitude and get rid of all negative aspects of our lives that have been holding us down for so long. We are sorrounded by wealth but yet we are blind to see it. We need vision and proper set of goals that within a time frame should be achieved and learn from the experience. Where should we start, since the current situation shows we are in a quagmire of corruptions, ignorance, technical know-how.

We should start from the roots of our problems, that is to understand where we are, where we came from, and where we should be going. In terms of poverty, we need to establish a system that will ensure the lives of our population is gradually but consistently improved. We can start from local authorities, every local authorities should know its natural and un-natural resources and how those resources benefit the local population. how many people live in the local area and how wealth is distributed among the individuals. Local authorities should have task-force groups that will ensure employment opportunities are explored in every direction and local people are given special priority in benefitting from their local resources.

A real example, let us take Kawe in Kinondoni District, the area is bordered with beautiful sandy beach with huge unoccupied areas. there are lots of young men without proper jobs and they involve themselves in day to day job hunting looking for any opportunity that may arise. some of them have formed a group for car washing along side the main road.

The local authority could use these young men and women for the benefit of the local area and the society in general by recognising their effort to employ themselves and provide them with facilities to officiate their work. The beach can be used as another employment opportunity by creating jobs like cleaning and maintaing the beach fronts and encourage people to visit the beach that will create a lot of informal business such as vendors for refreshment and entertainment goods.

Safety look-out for swimmers can be established and that will ensure the safety of all beach users. in the process the local authority can create an income by charging a small fee to the vendors who may operate on the beach front in peak time like saturday and sunday.

Official activities may attract people from other places to visit and hence increase wealth distribution among the local people for selling their services. all these process have to be transparent so that every element in the system know exactly what they are supposed to do.

Local authority initiatives can pave a way for its population to get rid of poverty with far more efficiency and positive results than what is currently being implemented.

Tuesday, 16 October 2007

Maendeleo Na Elimu toka Mwaka 47

Elimu ya tanzania katika ngazi ya shule ya msingi mpaka chuo kikuu inatia uchungu sana kutokana na ukweli kuwa haiendi na wakati. Wakati elimu ndio ingekuwa chachu ya kujua umuhimu wa kwenda na wakati, elimu yetu imebaki kama tulivyoachiwa na wakoloni.

Nashangaa hata huko chuo kikuu bado wanaendelea kutumia vitabu vilivyopitwa na wakati wakati teknolojia ya habari(IT Technology) imefungua milango ya elimu duniani ambapo wasomi wanaweza kubadilishana mawazo bila kujali kama wapo katika kona gani ya dunia. Elimu ya Uchunguzi (Research) katika mada mbalimbali ni muhimu kwa nchi yenye kujua umuhimu wa elimu ili kutatua matatizo yanayowakabili bila kusubiri kuiga kutoka kwa wageni .

Jawabu la tatizo fulani katika jamii fulani haliwezi kuwa jawabu la tatizo hilohilo katika jamii nyengine na hii inatokana na mambo mengi yanachangia kuwa na sababu ya kutafuta jawabo la tatizo hilo kwa kufanya uchunguzi kwenye jamii husika. Ni kosa ambalo kama msomi naliona likirudiwa mara kwa mara katika nchi za kiafrika ambapo badala ya kutilia mkazo kwenye kuboresha kiwango cha elimu watoayo kwa wananchi wao wamebaki ku-copy na ku-paste toka kwa nchi nyengine wakidhani itakuwa jawabu la matatizo yanayowakabili na hii inafanya nchi kuzunguka duara na kurudia kwenye tatizo lile lile badala ya kwenda mbele.

Nchi zilizoendelea zimeweka mkazo maalum kwenye vyuo vitoavyo elimu ya juu kuhakikisha kwamba research mbalimbali zinafanyika na kusaidia jamii kujikwamua katika matatizo mbalimbali yanayoikabili. Bila dhamira na Utekelezaji wa vitendo katika kuhakikisha elimu itolewayo ina manufaa kwa jamii husika Afrika hatutaweza kujikwamua katika dimbwi hili la Umasikini.

Thursday, 20 September 2007

Elimu na Mitihani.....

Mitihani ni kipimo cha maendeleo ya mwanafunzi katika masomo anayofundishwa, Mfumo tulionao ili uweze kwenda mbele lazima ufaulu mtihani wako wa mwisho katika kila daraja la elimu iwe darasa la saba, form four, form six ama hata mitihani ya mwisho wa semester chuo kikuu. Mara nyingi imejitokeza hali ambayo mitihani huibiwa kabla na kuuzwa kwa watoto wenye pesa ili waweze kukariri majibu na kuweza kufaulu kirahisi, hata imebainika kuwa baadhi ya shule kutumia wanafunzi waliokwisha maliza kufanya mitihani kwa ajili ya watoto wengine. hali hii iko katika ngazi zote za elimu..kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. matokeo yake ni kupata viongozi wabovu wasio na elimu ya kutosha ya kuweza kufanya maamuzi yatakayoleta maendeleo ya nchi. Japo juhudi za ujenzi wa sekondari kila kata ama wilaya utapelekea kuwa na shule za kutosha kukidhi mahitaji ya wanafunzi lakini kama hakuna vifaa vya kutosha katika shule hizo ama hakuna walimu wenye sifa za kutosha katika shule hizo, taifa litapata hasara ya kukosa Nguvu kazi stadi. Ubora wa elimu uzingatie mahitaji ya jamii.. jamii kwa sasa inahitaji madaktari, manesi, mafundi bomba, mafundi umeme, mafundi nyumba, na pia seremala, watengeza magari na pia watengeza vitu vya eletroniki. kama elimu itaanza kulenga mahitaji ya jamii na nchi kwa ujumla itaibua ajira na hivyo kuboresha maisha ya watu wake. KUIBA MITIHANI hakutaisaidia nchi bali kuiangamiza. PIA MITIHANI ISIWE KIPIMO CHA MWISHO CHA UWEZO WA WANAFUNZI, MAENDELEO YAO SHULENI KWA UJUMLA NDIO IWE KIPIMO , MARA NYENGINE UNAWEZA KUWA NA UFAHAMU MZURI WA MASOMO LAKINI KUTOKANA NA HALI INAYOWEZA KUJITOKEZA SIKU YA MTIHANI UKASHINDWA KUFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI HUO...

Monday, 10 September 2007

Tuanzie wapi...Things Do NOT Just Happen

Ndio, vitu haviwi tu hivihivi, tuanzie wapi, maana mpaka sasa hatujui tuko wapi na nina shaka kama bado tunakumbuka tulikotoka. kila siku maneno ya kupongeza maendeleo HEWA yanarushwa redioni, kwenye televisheni na kwenye mabango makubwa kuliko nyumba zilizokaribu na mabango hayo.

Tazama picha hapo juu halafu unambie kama walijenga tuu bila PLAN, kama hakuna mfumo maalumu wa kuhakikisha elimu, ubunifu unatumiwa katika miradi ya kuleta maendeleo hakuna kitakachokua, ndio maana kila siku utasikia mtaa fulani nyumba zitavunjwa kupisha ujenzi wa barabara, matokeo yake ni kupoteza pesa za taifa katika kulipa fidia kitendo ambacho kingeepukwa kama kungekuwa na mfumo wa kusimamia ujenzi mijini na mahala popote pale. watu wanajijengea kiholela kwasababu hakuna mipango ya ujenzi miji ndio maana nyumba zimeshikana kama matundu ya ndege hakuna njia ya kupita gari ama maeneo wazi.. ikitokea hatari msaada hauwezi fika kwa wakati.

HIVI MAOFISA KWENYE WIZARA YA ARDHI WANAFANYA KAZI GANI, MIAKA AROBAINI NA SITA LAKINI SIJAONA LA MAANA WANALOFANYA KUDHIBITI UJENGAJI KIHOLELA, NA SILAUMU WAJENGAJI KWASABABU HAKUNA MAELEKEZO TOKA KWA WAHUSIKA, UKISHA MALIZA KUJENGA KIBANDA CHAKO WAO WATAJIFANYA WATAALAMU WA KUJA KUBOMOA ILI WAKURUDISHE KWENYE UMASIKINI WAKATI TAYARI ULISHAANZA KUJIKOMBOA.

PITA MITAA AMBAYO TAYARI BARABARA ZIMEKARABATIWA NA KUWEKWA LAMI, UTAKUTA JAMAA WENGINE WANAKUJA KUCHIMBA MAHANDAKI WAKIMALIZA KAZI YAO WANAYAACHA WAZI AMA WANAWEKA KIFUSI, BADALA YA KUREKEBISHA KAMA WALIVYOKUTA...MWISHO MMOMONYOKO UNAHARIBU BARABARA NZIMA..WAHUSIKA WAKO WAPI..NANI ANAPASWA KUFUATILIA UTUNZAJI WA BARABARA?

WENZETU WALIO KWENYE NCHI ZILIZOENDELEA WAMEWEKA TARATIBU AMBAZO LAZIMA ZIFUATWE, NA PIA WASIMAMIAJI WA KUHAKIKISHA TARATIBU HIZO ZINAFATWA tena BILA RUSHWA , KATIKA KILA JAMBO KUANZIA UJENZI WA BARABARA, NYUMBA, HOSPITALI, MASHULE, MAHOTELI NA KILA KITU ILI KUHAKIKISHA UBORA WA MAISHA UNALINDWA NA KUENDELEZWA.

SISI RUSHWA NDIO MTENGEZAJI WA YOTE UNAWEZA KUPINDA CHOCHOTE ILI MRADI UNA PESA ZA KUHONGA..NAFIKIRI MUDA WA KUENDEKEZA MATUMBO UMEKWISHA SASA TUANZE KUJENGA MAENDELEO YA KWELI KWA KUONDOSHA KILA AINA YA UPENYO WA MIANYA YA RUSHWA PIA KUWEKA TARATIBU MAALUM KUSIMAMIA KILA KITU NA PIA KUWEKA WAZI TARATIBU HIZO ILI KILA MTU AJUE HAKI YAKE NA IWE RAHISI KUPATIKA KWA HAKI HIYO BILA YA VIKWAZO VYA UKIRITIMBA.

TUANZIE KWENYE ELIMU MAANA NDIO MAMA WA YOTE..MATATIZO TULIYONAYO NI KWASABABU YA UKOSEFU WA ELIMU BORA..NA NINAMAANISHA ELIMU BORA SIO HII TULIORITHI KWA WAKOLONI..


Friday, 7 September 2007

Upumbavu wa Mwafrika...Mbele ya Mzungu









Mniite Mbaguzi, lakini kwa hili lazima niseme, SHIDA ZOTE ZILIZOPO AFRIKA HII LEO ZIMELETWA NA WAZUNGU KWA NJIA MOJA AMA NYENGINE NA YOTE HII NI KWA AJILI YA KUJINUFAISHA WAO. Hivi niwaulize jamani huu utalii wa kuja na kuua wanyama katika mbuga zetu una faida gani je thamani ya maisha ya wanyama hawa ni pesa chache zinazochapishwa na hao hao wazungu, WANAKUJA na bunduki zao wakijifanya ni wawindaji, halafu na sisi kwa upumbavu wetu na kukosa akili tupo mbele kuwaongoza katika kuangamiza maliasili zetu, mbona kwao ukiuwa paka utalaaniwa na kila chombo cha habari kwamba wewe ni shetani hufai kuishi pamoja nao sasa leo iweje watoke kwao na kuja kwetu kwa kisingizio cha utalii ambacho tafsiri yake haina uhusiano na mauaji ya wanyama pori wasio na hatia. hawa si watalii bali ni waangamizaji wanaopenda kumwaga damu za viumbe bila sababu za msingi. TROPHY hunting ni upumbavu kwa binadamu mwenye akili timamu, nani kama si mwendawazimu anayependa kuona kichwa cha simba kilichotundikwa kwenye ukuta wa sebule anamoishi maana kama ni uhodari na ujasiri kwanini watumie bunduki kuua.
UTAJIRI ASILIA UMEKUWA LAANA JUU YETU, HATUNA UTAMADUNI WA KUTHAMANISHA MALI ZETU LAU KAMA INGEKUWA WANYAMA HAWA WAKO NCHI ZA ULAYA HAKUNA AMBAYE ANGETHUBUTU KUUA, LEO HII NCHI KAMA YA UINGEREZA, HUWEZI KWENDA PORINI KUTAZAMA MWEWE KAMA HUNA KIBALI CHA KUTAZAMA WANYAMA, SISI WAPUMBAVU TUSIO NA AKILI NA MAARIFA TUNAWATANGAZIA KUWA NJOONI MUUWE SIMBA, NYATI, TEMBO, CHUI ILI MRADI MTUPE PESA. PESA KITU GANI KAMA MASHINE ZAO ZA KUCHAPISHA HAZIJAWAHI KUZIMWA TOKA ZIANZE KUFANYA KAZI, WANATUMIA HAYO MAKARATASI KUCHUKUA MALI, NIPE DHAHABU NIKUPE MAKARATASI, NIPE ALMASI NIKUPE MAKARATASI, NIPE ARDHI NIKUPE MAKARATASI, NATAKA KUUA SIMBA KUMI NITAKUPA MAKARATASI....MAKARATASI YAKO HAYANA THAMANI YANGU TU NDIO YENYE THAMANI...KARATASI LANGU MOJA SAWA NA YAKO ELFU NA MIA MOJA....UPUUZI MTUPU.
HIVI KWANI MAENDELEO NI MPAKA TUWE KAMA WAZUNGU, TUVAE, TULE, TULALE, NA PIA RANGI ZA NGOZI ZETU ZIWE KAMA ZAO MAANA ZA KWETU TUNAONA HAZINA THAMANI, INABIDI TUJICHUBUE...
UWINDAJI NA UUWAJI WA WANYAMA KWA JINA LA UTALII UKOMESHWE KWA AJILI YA KIZAZI HIKI NA VIZAZI VIJAVYO...
HAWA JAMAA WAMEPOTEZA NA KUTOKOMEZA AINA NYINGI ZA WANYAMA KUTOKANA NA USHETANI WAO.. NA SISI JINSI TUNAVYOWASAIDIA TUTAKUWA KAMA WAO WANYAMA WATATOWEKA, TUBAKI PATUPU.






Thursday, 6 September 2007

Usafiri wa Mbagala Luxury Bus


You are very primitive if you have never boarded a luxury DCM daladala to Mbagala rangi tatu! I am very serious, you must be in another world altogether. YOU are not in Bongoland!!! Why dont you prove me right or wrong and take a trip from ferry to Mbagala? Or much better Mbagala to Mwenge or Kawe this weekend???? Back to Mbagala. So I did this experiment last weekend. Bored and hopeless I decided to just go to Mbagala, then Kongowe,then to Kibada, then Mji mwema, then Kigamboni, then board the dangerous MV Alina or Kivukoni ferry accross the ocean then a bus to Mtoni and call it a good and blessed day. That is a poor mans' tourism.Just go around, drink madafu and go back to your so called home! It is your home anyway, no matter if the roofing is made up of grass! The whole round trip costs only 2,000 bob .Tourism is not only about Manyara, Serengeti and Selous. I boarded a noisy and smoky TOYOTA DCM bus from Ferry to Mbagala Rangi Tatu and it was a trip to hell. I did not count but I could guess we were more than 80 in a 40 seat bus.This is bongo! Some of the passengers were getting through the windows and others were getting through the door! Nothing strange for Mbagala citizens! This is perfectly normal. Some young men were chewing sugar cane in the bus and several women had buckets of fresh fish, mostly sardines. Others were eating oranges and friedfish...that is total freedom!!! There were few young men smoking in the bus and no one dared to say anything!!! Say a word and you may end up in a hospital bed with several stitches on your scalp plus tetanus if you are not already caput. The bus was full but the conductor said there was a lot of space, just squeeze into the bus...once the head enters, you are inside!!!

"Kuna nafasi za kulala!!!siti bado kibaaaao, gari haijai, inajaa ndoo yamaji!!!""

Dont worry,some can even go up into the carrier. And there were not less than ten up there. They must pay 200 bob before they are allowed to climb the ladder to heaven. When at last the driver was convinced that even the door cannot be closed, we started our luxurious trip. There were fumes of all kinds...alcohol, cigarettes, fish and of course some exhaust from some places and holes.

"We dada uwe unanyoa j amani !!! Mrembo mzuri lakini kikwapa kinanuka!!!" "Mpashe huyooo...kasuka nywele utazania kalambwa na ng'ombe!!! Eti ndio katoa shilingi alfu saluni! mie kama ni mke wangu namnyoa usiku...zooote akiamka kama kibwengo!!"

"Mrembo gani huyu hebu mwone midomo kama subiani...hivi anajiona kapendeza sanaaaa!!! Eti wanaiga wazungu lipustiki!!!" " Kama ni mke wangu wallah nakuapia talaka saba!!! Ati anajifanya misstanzania ...kumbe kalalia mlo wa mhogo na mchicha!!!"

I knew something was brewing...not good!!! A middle aged man at the back seat began to vomit...and it was nasty!!! "Eheee!!! gongo la kigamboni hilo !!!." Kwani Kigamboni kuna gongo la bure??? Pesa yangu nakula...nitakutoa nishai... Wee kama huna hela shauri lako macho kama kenge kasoro mkia etcetc.. We pretended not to laugh ,lest the wrath of the devils turn upon us.

We mama mbona unanikalia? na minguo yako imelowa misamaki???unajua bei ya hii suruali yangu?? Umewahi kukaliwa weee,koma kabisa!!! kama una ubavu si ushuke ukapandetaxi??? Wee mama si ungepanda ungo,mwanga mkubwa wee!!!

and so on and on and on!!! We ended up at Kilwa Road Police station!!! Not from the foul and filthy language and insults but from a totally different story. The so called conductor, who I can tell you never attended any school,began collecting money straight away. As usual some young snake- generation (mzao wa nyoka?) skin head,pretended that he was deep asleep, of course after taking cheap gongo at Kigamboni. The conductor woke him up roughly demanding bus fare. The red eyed son of the earth , with a pungent smell of a mixture of cheap alcohol retorted "I dont have a single cent! You can go to hell" The conductor was not a fool. He went around collecting other passengers fares and went back to the red eyed young devil. This time everyone knew that a something terrible would soon happen. He took the drunk by the collar and demanded money. The young devil produced a knife and the conductor produced a screw driver, and it was a madmans'house.

"Dereva peleka gari polisi!!! Kuna mchizi hataki kulipa halafu anakisu!!!Lazima aende selo huyu!! "

By then we were near police station, Kilwa road.The driver took the overloaded bus to Kilwa road police station.Someone in the bus said: "hivi kweli abiria tunapelekwa polisi kwa ajili ya shilingi mia mbili tu?? Mimi nitamlipia!" The bus had already parked. A policeman came and asked what was the big deal! "Afande kulikuwa na Chizi hataki kulipa lakini mimi nitamlipia!

"Come on...did you come for fashion show at a police station?Everyone in the bus come down, one by one and you driver come and write a report inside.

"Mmekuja kuuza sura hapa? gari imejaa kama ile ya Mererani, nanyi abiria mnakubali kupangwa kama sangara!!!Halafu unadhani utaondoka hivi hivi tu hapa? Gari yako kwanza ni mbovuna hii ni wiki ya usalama haijakaguliwa!!!"

The man who was vomiting could not come down. He alone was left at the back seat of the bus ,snoring! We spent more than one hour under police watchful eyes and at last we were allowed to board our beloved bus... I dont know what the driver did but there was a very good smile onthe policemans face when we were leaving, he even wished us safari njema!!!Bon voyage. Jaribu na wewe kama huamini. I remember someone in high places mentioned "MABASI YA KASI"... or was it adream??? Yanakuja lini? Karibu Mbagala...au ELEKEA KAWE.

Ningelikuwa Mwalimu MKUU wa Shule...

Ningehakikisha kwanza majengo ya shule ni ya kuvutia ya na Milango na Madirisha, kuta zimepigwa rangi na pia madawati ya kutosha kwa kila darasa. Pia darasa lisizidi wanafunzi Arobaini na tano. ningehakikisha kuna Maktaba ya Vitabu na Vitabu vya kutosha kwa ajili ya wanafunzi na walimu. Kuna Viwanja vya michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu(football), Kikapu kwa waume na wanawake(basketball and netball), pia na riadha. hakikisha walimu wako na elimu inayokwenda na muda kwa kuhamasisha upitiaji wa majarida ya kisasa yahusuyo elimu ya nadharia na pia vitendo. ningehakikisha kuna Maabara na pia karakana kwa ajili ya mafunzo ya vitendo yakiwemo ya ujenzi, seremala, uchongaji, kilimo, ufugaji, ufundi wa magari, vitu vya elektroniki na aina zote za ufundi ambazo hawa wanafunzi wakimaliza shule wawe na uwezo halisi wa kujitegemea. ningehakikisha walimu wanalipwa mishahara yao kwa wakati muafaka, pia wanapongezwa kwa juhudi binafsi wanazojitolea. ningeweka mkazo maalum katika kuhakikisha jamii inayozunguka shule hiyo inafaidika na pia shule inafaidika kutokana mahusiano mazuri kati ya shule na jamii husika. ningehakikisha wanafunzi wanawekewa mazingira ya kuipenda shule na kusaidia wanafunzi wasio na uwezo kupata elimu sawa bila ubaguzi wa aina yeyote ile. ningehakikisha kuna heshima na maadili bora ya kazi kwa wote wanafunzi na walimu pia. ningehakikisha kuna safari za kimafunzo kama kutembelea mbuga za wanyama ili kujifunza mahusiano ya binadamu na wanyama mwitu pia uhifadhi wa mazingira, kutembelea viwanda kujifunza jinsi bidhaa zinavyozalishwa na pia mashine zinavyofanya kazi. kuweka mashindano ya ubunifu wa vifaa na vitendea kazi, uboreshaji huduma na mambo mengi ili kuibua mawazo mapya kusaidia jamii kujikwamua toka kwenye matatizo yanayoikabili.

Wednesday, 5 September 2007

Kama ningelikuwa ...MWALIMU darasani

Ningefundisha masomo yatakayosaidia kuinua jamii toka kwenye dimbwi la umasikini. ningerekebisha mitaala isiyo na manufaa na wanafunzi, ningependekeza elimu vitendo zaidi ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa wabunifu katika masuala mbalimbali badala ya kuwafundisha kukariri vitabu. ningehakikisha natumia vitabu vya kisasa zaidi ili elimu nitakayotoa iwe inakwenda na wakati. ningewapa wanafunzi uwezo wa kutumia akili zao katika kutafuta majawabu ya matatizo yanayoikabili jamii kila siku na pia kuhakikisha mawazo yao yanafanyiwa kazi kwa vitendo. ningefundisha madhara ya rushwa kwa jamii ili wanafunzi hao waichukie kwa kuwa ndio adui wa maendeleo yao. Elimu tuliyonayo sasa ni ile tuliyoirithi toka kwa WAKOLONI, ambayo lengo lake ilikuwa kuelimisha wachache ili wawe vibaraka na jamii ilobakia iwe ni wenye kuongozwa bila kujua haki zao na wabaki kuwa ni wafanyakazi katika kunyonya mali za nchi yetu kwa manufaa ya WAKOLONI hao. ELIMU ya Mkoloni imejengwa kwa mfumo wa piramidi, pana ukianzia chini na hupungua kuelekea kileleni. WANAFUNZI milioni huandikishwa shule za MSINGI ili wakimaliza wajue KUANDIKA NA KUSOMA tu. wachache hata wakifaulu mitihani ya DARASA LA SABA inabidi wachaguliwe wale wanaoonekana kufaa kuendelea elimu ya sekondari. hapo ni asilimia 10 ya wote waliofanya mitihani ndio wataoendelea na elimu ya SEKONDARI, waliobaki watarudi nyumbani kuwa wakulima, wavuvi, wabeba mizigo, WEZI,na MAJAMBAZI. hao waliobahatika kwenda sekondari watachujwa baada ya mtihani wa FORM FOUR, ambapo pia ni asilimia isiyozidi kumi watakwenda FORM FIVE na SIX, na baada ya hapo wachache watachaguliwa kwenda vyuo vikuu. JAPO TUNAONA MABADILIKO LAKINI HATA MITAALA ITUMIKAYO SASA NI ILE YA WAKOLONI, VITABU VITUMIKAVYO VIMEPITWA NA WAKATI, HAKUNA USIMAMIZI WA KUTOSHA WA KUANGALIA UBORA WA ELIMU TUIPATAYO, WENGI WANAMALIZA FORM SIX NA ENGLISH BADO YA UGOKO. HAO WANAOPELEKWA NJE YA NCHI KUSOMA KOZI MBALIMBALI HAWANA JIPYA WAKIRUDI NYUMBANI KWASABABU MUDA WOTE WAO NI DARASANI, CHUMBANI HAWANA FIKRA ZA KUTOKA NJE YA VYUO KUONA JINSI WENZETU WALIVYOTENGENEZA BARABARA, HOSPITALI, MASHULE, NA MAMBO AMBAYO WANGEWEZA KUJA NA KUIGA ILI KUTULETEA MAENDELEO HAKUNA LABDA WATAKUJA WATULETEE MAMBO YASIO NA MAANA KAMA KUIGA MAMBO YA BIG BROTHER, NA UPUUZI MWENGINE USIO NA MANUFAA KWA JAMII.
ningetumia elimu yangu kubadili mazingira yanayoizunguka jamii yangu na kuweza kutoa chachu itakayoleta mabadiliko katika jamii katika kila nyanja, kama vile kubuni mbinu za kutoa ajira kulingana na mazingira, kuboresha huduma zitolewazo kwa jamii, kuweka wazi mambo na kutumia elimu katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii. je wewe ungefanyaje?

Monday, 27 August 2007

Urithi wetu Asilia Unavyo Yoyoma

Vitabu vya dini vina himiza waliopewa dhamana ya mali ya watoto yatima kuwa waangalifu na waadilifu tena wasitumie mali kwa kufuja na kujinufaisha wao binafsi. sisi watoto wa watanzania ni sawa na hao yatima na viongozi wetu ndio wenye dhamana ya kututunzia utajiri wa asili tuliojaaliwa na Mwenyezi Mungu ili tuje kunufaika tutakapo kuwa tayari kiuwezo na kielimu kuvuna maliasili zetu ili tuondokane na umasikini huu wa kujitakia. Mimi SI mwanasiasa lakini hupenda kutumia bongo langu kufikiria, hivi kama kweli viongozi wetu wana nia ya kututoa katika umasikini kwa nini isisomeshe wabongo katika fani hii ya uchimbaji madini na kuweza kuunda mashirika ya serikali katika uchimbaji, usafishaji wa madini yetu badala ya kuuza ardhi yenye shehena ya madini kwa wawekezaji ambao wengi wao hawana uchungu na nchi yetu na lengo lao kuu ni kuchukua madini na kujinufaisha na wala sio kutuendeleza na kutusaidia kuondokana na dimbwi hili la umasikini. Kwa hesabu ndogo tu kama matarajio yao ya chini ni kuzalisha 2.6 million Ounces za Dhahabu (hii inatoka kwenye website ya Barrick Gold kwa Mgodi wa Buzwagi), kwa sasa soko la dunia Ounce Moja ya dhahabu ni zaidi ya Dola 600, Piga hesabu mwenyewe wakati wao wametumia millioni 400 USD utakuta ni 1.6 Billion USD ukitoa gharama za kuzalisha Ounce moja ya dhahabu utakuta faida yao ni asilimia 200 za msingi waliotumia hapo huja taja matarajio ya Tani elfu 54 za Copper zilizopo hapo mgodini na hayo NI makisio ya chini. Ukiangalia taathira za uchimbaji huo kwa jamii inayozunguka migodi hiyo ni hakika kuwa mabadiliko ni machache katika uboreshaji wa maisha ya wananchi. Migodi ni sehemu moja tu ya utajiri tuliojaaliwa kuwa nao kuna mbuga ambazo kabla ya wazungu kuja afrika kulikuwa na mamilioni ya wanyama wa aina tofauti lakini leo tumebaki na mamia ya wanyama na kila siku hao waliobaki wanahamishiwa kwenye MA-ZOO nchi za ulaya kwa kisingizio cha kuhifadhiwa dhidi ya majangiri, lakini ukweli ni kwamba itafika siku ukitaka kuona wanyama mwitu itabidi uende Ulaya uone wanyama tena kwa kuwalipa pesa SI BURE. Kutokana na hali ya Usalama kutokuwa ya uhakika katika nchi nyingi za afrika ikiwemo Bongo watalii wengi huenda kuona wanyama kwenye MA-ZOO Ulaya na hata wameanza kujenga mifano ya mbuga za afrika huko AMERIKA tena kwa kufuatilia kila detail ya mbuga kuanzia vichuguu mpaka mito na mabonde mpaka vibanda vya wamasai na wamasai wenyewe kiasi itafika kipindi watu wataenda SERENGETI YA BUSCH-GARDENS iliyoko Marekani kwasababu inawanyama wengi kuliko Serengeti halisi iliyoko afrika. VIONGOZI WETU KUWENI WAADILIFU NA WAONA MBALI, KUUZA MALIASILI KWA BEI YA MLO WA SIKU MOJA INATUANGAMIZA SASA NA HAPO BAADAYE. TUJIFUNZE KUTOKA KATIKA NCHI KAMA DUBAI, MALAYSIA NA KWENGINEKO AMBAKO MIRADI YAO NI KUENDELEZA NCHI NA WANANCHI WAO NA SI VINGINEVYO. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA AFRIKA PIA.

Friday, 24 August 2007

Taxi yenye Horsepower ya Kweli


Haya nyie mnaotaka kupunguza GLOBAL WARMING, Mjionee wenyewe njia mbadala za kufaidi utamu wa gari bila kuumiza mazingira. picha hisani ya mdau mmoja anayependa usafiri ambao ni eco-friendly.

Monday, 20 August 2007

Tutazame Utoaji wa huduma za Afya...

Jua limeshachomoza na harakati za kutafuta mlo wa leo zilishaanza mapema wavuvi washaelekea baharini na nyavu zao, wakulima nao njiani kuelekea mashambani. Wanafunzi vituoni kusukumana na makonda wa daladala kuelekea shuleni.

Katika mambo muhimu ambayo yanamhusu mwanadamu popote alipo ni huduma za afya hasa ukizingatia huku uswahilini ikipita miezi mitatu hujaugua Malaria ni bahati kubwa maana Mbu hushambulia hata ukiweka neti ya dawa mbu nao siku hizi huimba "ALUTA KONTINUUUUAaaa", na ukiamka utakuta wamejaza kibao ndani ya neti matumbo yao mekundu yamejaa mlo wa damu yako.

Uswahilini hakuna bima ya afya, DINGI anasema nikakate bima ya afya wakati BIMA ya Mlo wa Mchana sina. ndio hivyo ukiumwa huna budi kwenda kumuona daktari baada ya maji ya Mwarobaini kushindwa kukutetea dhidi ya mashambulizi ya vimelea ya Malaria. Hapo ndipo kasheshe linapoanza maana kabla daktari hajakutupia jicho inabidi ulipe ili macho yake yafunguke. na hapo baada ya kulipa hicho kiingilio cha kuonekana na daktari ndipo utasikia "HAYO NI MALARIA TU!!", anakucheki kwenye magoti huku akikuuliza "je UNASIKIA UCHOVU KWENYE MAUNGO?" .Na jibu ni lile lile la ndio na ukibadilisha hakuna mabadiliko katika vipimo nenda kapime damu pale kidirishani, ukienda hapo kidirishani kuna " MICROSCOPE" Imechoka na hata ya pale shuleni kwetu ina nafuu, jamaa akishakutoboa kwenye kidole anaweka chini ya kioo cha darubini yake huku akifinya jicho kuchungulia kilichomo, baada ya sekunde kadhaa utakuta keshaorodhesha mpaka idadi ya vimelea alivyokuta ndani, "Haya Tayari Nenda Kamuone Daktari".
Ukifika huko kwa daktari, hicho cheti chako ataandika kwa mwandiko ambao ni yeye tu na manesi ndio wanajua kusoma sasa nauliza kwani "KUNA SIRI GANI KWENYE CHETI CHA HOSPITALI MPAKA MUANDIKE KAMA CODED MESSAGE", miandiko kama kapita kuku, kila mwandiko ukizidi kuwa mbaya ndio daktari anajisifia kuwa ndio daktari bingwa, na dozi ni ile ile SINDANO, NA MIDONGE YA FANCIDA. wakati mwengine namwambia dingi ni bora tutumie cheti cha miezi mitatu ilopita maana tiba na ugonjwa ni uleule, badala ya kwenda kulipa kiingilio halafu juu yake ulipie matibabu. Ndio maana wananchi wengi hukimbilia kwa Waganga wa JADI kwa kuwa hakuna kiingilio japo hao WAGANGA WA JADI wakiumwa hukimbilia hospitali..
Na hapo umeumwa malaria tu ukienda kulazwa hospitali za wilaya utaona jinsi wagonjwa wanavyo-share vitanda bila kujali ugonjwa uliowapeleka hospitali. Manesi wanajitahidi kutoa huduma lakini hakuna motisha wa kutosha wakuwafanya wapende kazi yao, Mie nadhani hufanya kazi ile kwa mapenzi na huruma waliyonayo ndani roho zao na si vinginevyo kwa maana mishahara yao haikidhi mahitaji yao.
Madaktari wao afadhali wanafanya kazi mbili kwa wakati mmoja, Kaajiriwa na hospitali ya serikali lakini muda wote yuko kwenye hospitali yake uchochoroni, ukiulizia utaambia daktari hayupo lakini ukionyesha noti utapewa maelekezo aliko huko kichochoroni.. ATAFANYAJE WAKATI AKILILIA ONGEZEKO LA MSHAHARA serikali inamfukuza kazi, si bora awe anafanya Overtime pembeni UKIZINGATIA ana familia na extended-familia na marafiki pia wanamtegemea. Na hayo ndio mambo SIKU ZOTE OMBA AFYA NJEMA ndio jambo muhimu..

Thursday, 16 August 2007

Uwekezaji au Uchukuaji...


Kuwekeza kwa maoni yangu kuwe na manufaa na mahala panapoekezwa iwe ni mgodi, kiwanda, nyumba ama kitu chochote kitakacholeta manufaa kwa wanaouzunguka hicho kilichoekezwa, kwa mfano kila unapochimba mgodi kuna matokeo mawili, la kwanza ni kupatikana kwa kile unachokichimba na pili ni uharibifu wa mazingira ya hapo ulipochimba. kama ujuavyo kila mchimbaji huacha shimo kama kilichochimbwa hakitarejeshwa mahala kilipokuwa. Uharibifu wa mazingira katika migodi ni wa kudumu kwa hiyo lazima fikra za kuweza kujaribu kuziba uharibifu huo lazima upewe kipaumbele kama jamii izungukayo migodi hiyo iweze kuendelea kwa kutengenezewa vipato mbadala ili mgodi unapokufa pawe na njia nyengine ya kupatia ajira hao wafanyakazi na pia hao wanaozunguka mahali hapo. kama dhahabu, almasi na madini yote yatakwenda kusafishwa nje nchi pesa ambayo ingepatikana katika shughuli za usafishaji huo hazitopatikana na badala yake itakuwa ni uchukuaji na si uwekezaji tena. na matokeo ya uchukuaji ni kuachwa kwa mashimo matupu ardhini ambayo ni hatari kwa mazingira ya mahala hapo. Kama kweli ni wawekezaji basi waje na kitu kamili, wajenge mitambo ya kusafisha, wajenge maduka ya kuundia vito hapo hapo penye kuchimbwa madini hayo na sio kuyachota na kuyapeleka kwao na kuyapa faida zaidi(value added) wakishayaunda kuwa vito vya thamani ama kwa matumizi mengine. wakijenga mitambo itakuwa ni ajira kwa wazawa, wakijenga maduka tutapata ajira na miji itakuwa kutokana na faida ya wanunuzi toka nje wakinunua kitu kilichoongezewa thamani na hivyo kulipa taifa faida zaidi na kuinua hali za maisha za wananchi wake tofauti na ilivyo sasa. tujiulize kwanini dhahabu ichimbwe afrika ikasafishwe ulaya...sie tuuze bei ya mchanga wao wakauze dhahabu huu ni ujinga wa hali ya juu, bora ibaki ardhini mpaka tutakapo kuwa tayari kuichimba wenyewe kuliko kuibiwa hali tuko macho...

Wednesday, 15 August 2007

SOMETIMES I CRY.......AND



I now know Why Millions of People cried when He Died, To tell you the truth I was not fond of Him, I was Young and Stupid, those mourning days were long and tiresome for me so i was busy watching Movies, Mind you i live in those slum like residential areas where there is no street houses built to make shanty towns where alleyways are full of dirty running water emanating from nearby pit latrines, foul smell everywhere but who cares we were born there so i guess we got inbuilt biological immunity against all vermins that thrived in those stagnant water full of mosquito larvae.

Lucky Me I had sold enough cup of teas and Ginger-laced drinks during school holidays to buy my first investment, a 21 inch TV and a VCR(Video cassete recorder and player), I had to buy it even though we did not have electricity in our house, You might ask why, i got tired to lie to my friends at school when they asked whether i had seen Isidingo the night before, obviously I said Yes with no details on what happened apart from blatant answer that it was rubish,before they could ask to elaborate. My investment yes because we had extra room that my father had envisaged to run a hotel, the venture that never went far because He could not balance his books that he spent more than he could earn. When the hotel went bust, i guess there WAS no enough customers to afford buying the food...SO I used that room for my Video shows, yes We will be showing First Blood by Rambo, kids from the block flocked in like flies to the you know What!, I got some school money from it so that i could afford a piece of cassava during the break time at school.

30 days of mourning was like Hell to me I could not show Pirated Movies anymore meaning my pocket was also in Mourning Mode. on 27Th day i decided to break the Mourning period because i could no longer take it the whole of my school funding was depending on video show, so i went and picked Commando video cassette by Schwarzenegger, before the movie could even finish the preamble so that we can start watching, Knock knock on the door, Two mean looking Policemen had arrived on the scene looking so furious that i thought my living days were over. "AROOOO MUNAANGARIA VIDEO RA SHWAZINIGA WAKATI BABA WA TAIFA AMEFALIKI" one of them growled, "NANI MWENYE HIRI VIDEO" one of them added, my stomach went grogrororor i could feel wind passing out my behind as I was strugling to reveal that i was the owner of the show... one of them quickly went and took the cassete out as evidence, lucky me they could not believe that i was the owner they resorted to take my dad to the police station for further enquiry, But I asked my self we have been watching the mourning sessions, histories, procession and mourning songs for 27 days on TV, we are not allowed even to earn some money...Any way They let him free after paying them a certain amount off-camera before they could reach the police station which was about 500 metres.

Now I know why people wept, to see all what they fought for being given for free to foreigners while they starve.

Wananchi wept because Leaders are lying to their faces that the country does not have enough money to go around while they build villas, mansions and palaces and ride on Mercedes, Lexuses and VXs.

Wananchi Wept because they can't afford to walk because of hunger let alone to pay for DalaDalas leaders opting to fly because the road is too bumpy for their royal bottoms.

People wept because after 46 years of being free they still live in the shacks they were promised to be moved from to better life, they can't afford to send their kids to school even though many building have been buit for the purpose.

Wananchi WEPT because they Knew that THEY WILL BE BULLIED AND there WILL BE NO one to STOP it.

IT IS LIKE WHEN DAD GOES ON SAFARI, KIDS ASSUME LEADERSHIP DO ALL THE MISCHIEF WHILE THE TIME LASTS, ONLY THIS DAD WILL NEVER COME BACK ONLY MEMORIES AND NO ONE TO ENFORCE HIS TRUE LEGACY.

AND THAT'S WHY SOMETIMES I CRY.....

Hivi Mwalimu Hakujua.....

Kama Tanzania ni nchi yenye Madini, mafuta, gesi, ardhi yenye rutuba, maliasili kwenye mbuga, mbona hakubinafsisha kwa kasi mali hizo wakati alikuwa na nia ya kuinua maisha ya wananchi wake..? Ukiangalia historia yake kuna ukweli tosha kuwa alijua hayo lakini pia alijua dhamira ya hao wawekezaji toka mataifa ya magharibi.. MFUMO WA UCHUMI WA NCHI ZA MAGHARIBI NI UNYONYAJI KWA GHARAMA YEYOTE ILE..

Pia Nafikiri alijua kwa hakika hakuwa na wasomi wa kutosha wa kuweza kusimamia miradi itakayotumia malighafi tulizonazo kwa hiyo kwa busara zake akaweka Kipaumbele kwenye Elimu ili tukishapata wasomi wa kutosha ndipo tuanze kutumia utajiri wetu asilia. Cha Kushangaza leo hii Nchi imesahau umuhimu wa elimu na kuacha watu wakijiita Madokta wakati hata darasani hawajaingia, watu wenye Vyeti feki wakijitamba kuwa sio lazima uwe na elimu kuongoza ama kuleta maendeleo, hawa hawa ndio wanapewa madaraka na kutokana na ukosefu wa elimu wanaingia Mikataba na watu waliobobea katika ku-(manipulate) kutumia ujanja ili kujinufaisha zaidi hali ya kuwa wenye mali wanabaki kuwa waangaliaji tu bila kufaidi mali yao. Nina Uhakika wale waliopokonywa mashirika baada ya uhuru wamerudi kwa kasi kuvuna kilichobakia kwa kasi mpya kabla ya watu hawajastuka. Elima ni kifungua macho na pia inawezesha kuona mbali zaidi ya mlo wa siku moja..

VIONGOZI WANABINAFSISHA MIHIMILI YA UCHUMI WA NCHI KWA AHADI YA MLO WA SIKU MOJA...MAJUMBA MAKUBWA YENYE KWENDA HEWANI, JUMBA LA BUNGE LA GHARAMA SIO KIPIMO CHA MAENDELEO YA NCHI...KAMA MALI YOTE INAMILIKIWA NA WACHACHE WAKISHIRIKIANA NA WAGENI... TULIOBAKI TUFANYE NINI.?..

MISHAHARA DUNI KWA WAFANYAKAZI NI KWASABABU HAKUNA ANAYEJALI KWAKUA PESA ZINAZOPATINA NI ZILE ZITOKAZO NJE na kukandamizwa wafanyabiashara wa ndani. NANI ATAJALI MFANYAKAZI AMEKULA NINI, MZOA TAKA BARABARANI AMESHINDA VIPI, MANESI HOSPITALINI NA WAGONJWA WAKO HALI GANI..

WABUNGE NI WASAHAULIFU TENA WASHABIKI WA VYAMA NA SIO MASLAHI YA WANANCHI WALIOWAWEKA BUNGENI..PENGINE HUONA FAHARI WAKIPITA KWENYE MITAA ILIYOCHOKA NA KUNUKA HUKU WAO WAKILA VIYOYOZI NDANI YA MASHANGINGI YAO TINTED...

MWANANCHI WA KAWAIDA NI SHIDA TU KWENDA MBELE BEI YA KUWASHA KOROBOI IMEPANDA BORA TULE KABLA YA JUA HALIJAZAMA LA SIVYO NI GIZANI MPAKA ASUBUHI..NA HIYO NDIO HALI BAADA YA MIAKA 46 YA UHURU...PENGINE TUKUMBUSHWE SABABU ZA KUGOMBEA UHURU MAANA WENGINE TUMEZISAHAU...

mpaka MLALAHOI atakapojua ATAKULA NINI KESHO KABLA JUA LA LEO HALIJAZAMA hapo ndipo tutakuwa tumepiga hatua....

Monday, 6 August 2007

Tutaijenga Hosteli Kwa Mikono Yetu Wenyewe....

Nguvu tunazo, mawe tunayo, nia ya kujenga hosteli tunayo tunachohitaji ni msaada tu wa kiufundi. Wanafunzi hawa walishiriki kujenga hosteli ya wasichana shule ya Mukulat Pale Ngaramtoni huko Arusha.

Na madada hawakukaa bali walisaidia mno katika kutafuta mawe kwa ajili ya msingi wa jengo hilo kama wanavyoonekana kwenye picha.

Huyo ni fundi aliyesaidia kuweka sawa msingi wa jengo ili uwe imara, Mtaji wa Masikini ni Nguvu zake na Mtaji wa Shule ni wanafunzi wake...


Matokeo yake...Ni Hosteli ya nguvu iliyojengwa kwa nguvu za wanafunzi, kama kila mwaka shule zingekuwa zina miradi ya kujijengea miundo mbinu kama hii tungefika mbali mno...Hapa cha kujifunza ni kwamba Waafrika Tuamke sio kusubiri misaada(Hand-outs) tunaweza kufanya mambo kwa kutumia malighafi tulizonazo tunachohitaji ni fikra tu jinsi ya kuligeuza jiwe likawa nyumba. Misaada bila fikra tutabaki ombaomba daima..



 

free counters
eDiets.com Weight Loss

Afrigator