Thursday, 2 August 2007

Je Watambua Kuwa.....


Simba dume halei watoto wa kambo. Simba dume akishafikia Umri wa kuweza kuzalisha hutoka na kuiacha familia yake alikozaliwa na kwenda kutafuta familia nyengine kwa lengo la kujenga familia yake. katika hatua hii kama katika familia atakayofikia kuna simba dume pia basi yule simba atapigana na huyu simba mvamizi na akishindwa itabidi akimbie ama auawe ili simba mvamizi achukue hatamu za familia. Kama kuna watoto wachanga kwenye familia hiyo simba dume huwauwa watoto wote ili simba majike yaweze tena kuzaa na huyo simba mvamizi..Na kwa hiyo Simba halei mtoto wa kambo...Je ulikuwa unajua haya?


No comments: