Monday 30 July 2007

Jengo la Shule-Tunajifunza nini?


Shule ni mkusanyiko wa majengo, wanafunzi, vitabu, walimu na mambo mengine, kama elimu itakayotolewa katika jengo hili ina manufaa na jamii mbona jengo lenyewe halionyeshi manufaa hayo. Maana jamii ikielimika majengo yatakuwa mazuri, mazingira yatakuwa safi, barabara zitakuwa zinapitika wakati wa majira yote, na ubora wa maisha ya jamii itakuwa juu kwa ujumla, leo iweje majengo kama haya hata madirisha hayana yaweze kutoa wasomi watakao endeleza nchi?. Kujenga shule mpya sawa lakini je zile za zamani mtazifanyia lini ukarabati au mpaka zianguke ili tujenge upya, maana msemo unasema asiyeziba nyufa atajenga ukuta. wana jamii tuelewe maendeleo ya jamii huletwa na wanajamii sio kusubiri serikali.

1 comment:

Anonymous said...

blogu yako inapendeza, hongera.