Thursday 2 August 2007

Kibanda cha Babu...Milima Ya Kwetu


Kibanda cha babu, kila ninapo mtembelea nakuta vigoda vinaongezeka, Vijijini wanawake hufanya kazi zote kuanzia kutafuta kuni, kuchota maji umbali mrefu mno, kulima shamba, kuvuna, kutafuta mboga, kutwanga mpunga au kusaga mahindi, kupika, kulea watoto. Wanaume kazi yao ni kupiga Stori na kupiga Ulabu kuanzia asubuhi mpaka usiku. Unafikiri kutakuwa na maendeleo hapo... na huu ni ukweli hata kama hutaki.. na ninajua kuwa ukweli unauma..

2 comments:

Anonymous said...

Mwanafunzi

Tanzania ina jamii nyingi sana. Sijui wewe hilo la wanaume wanapiga stori asubuhi mpaka jioni umelitoa kwenye jamii ipi. Sikatai kama ni kweli kuna jamii za aina hiyo ila ku-generalize mambo nafikri sio vizuri. Mimi nimeishi kijijini tangu utotoni mpaka nilipokuwa na miaka 22. Kwetu, tulikuwa tunaenda shamba wote, na ikifika mida ya saa 5 mmoja wa akina mama anaenda nyumbani kuandaa msosi, ikiwa ni pamoja na kuchota maji. Sisi na wamama wengine tunaendelea na kazi. Baada ya hapo tunaenda kula na unakuta mwanaume anaondoka kwenda kuchunga ng'ombe mpaka jioni. Kuvuna tunavuna wote na mara nyingi kwetu wanavuna wanaume zaidi. Kupiga mahindi au mtama au mpunga mara nyingi kunafanywa na wote na zaidi wanaume.

Sijui labda ulete uzoefu wako umeuchukulia wapi. Hili nimekupa ni la jamii za watu wa Singida. Nawe mwaga mfano wako hapa

Anonymous said...

Kweli wanawake wanafanya kazi nyingi kuliko wanaume huku wanaume wakijikatia pande kubwa kuliko wanawake...ila kweli inategemea na sehemu ila kwa ujumla vijijini wanawake wanafanya kazi kuliko wanaume.