Friday, 3 August 2007

Marashi Ya Karafuu...Nitakwenda Pemba

Nasikia kuna Upepo, Tena Unanukia Marashi ya Karafuu, Nipae Angani, Nivuke na Bahari kisha Nitue Pemba, Pemba OOOOH Pemba...Jamani wa Ughaibuni hebu tazameni tulivyojaaliwa bahari yenye mchanga mweupe, bahari safi, bluuuu yenye kupendeza machoni.. Njoni kupumzika nyumbani wakati wa holiday zenu za makazini, hamjui nyie kuwa mchumia juani hulia kivulini...Njoni muone madhari ambayo hamkuiona wakati mlipokuwa huku kwasababu ya shida na mambo mengi lakini sasa mmeshasafisha macho njoooni muogelee na dolphins sio wazungu pekee wenye uwezo hata nyie pia.. njooni muendeleze utalii wa ndani....Njooni munywe maji ya madafu kwa mrija...Mkija nyie na sisi tunapata faida tena kubwa sana.

No comments: