Friday, 3 August 2007

Je Wajua Kwamba Red Colobus Monkey au Kima Punju

Hupatikana Afrika mashariki pia ni aina ya kima ambao ni wachache sana hapa duniani hupatika katika msitu wa Gombe Ulioko Tanzania Bara na Msitu wa Jozani Ulioko Zanzibar(unguja). Watalii na wanamazingira toka nchi za ulaya hutembelea misitu hii kujionea wanyama hawa adimu. Kuna mashirika yaliyoundwa rasmi kwa ajili ya kulinda wanyama hawa dhidi ya waharibifu. Je shuleni kwenu umewahi kusikia mpango wa kwenda kutembelea mbuga ama hifadhi ili kujionea wanyama, kama bado fanya ushawishi ili muende kuona utajiri asilia tulionao sio kwa wageni tu toka nje ndio waone tuliyonayo wakati sie wenyewe tunasikia kwenye hewa. Kila mwaka shule nyingi zilizopo Amerika (USA) huleta wanafunzi kujionea wanyama katika mbuga za Serengeti na nyenginezo huku wakifanya utafiti mbalimbali na kujifunza mengi kutokana na safari hizo, Kwa nini Wizara ya elimu haiweki mkazo katika suala hili maana kama Watoto wataona jinsi wanyama wanavyoishi katika jamii zao mbalimbali (maana usifikiri ni binadamu tu ndio wenye kuishi katika mfumo unaotambulika) jinsi wanavyotafuta kiongozi wa kikundi ama familia na pia jinsi wanavyosaidiana katika maisha ya kila siku basi tungeweza kupata watu watakao linda mazingira yao na hivyo kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinafaidika na maliasili hii...Changia usiogope..Kuchangia ni kuelimishana..

No comments: