Monday, 6 August 2007

Elimu Bora na Ukaguzi wa Majengo

Katika pitapita yangu huko mikoani nilikuta shule hii, sikuona wanafunzi labda kwa kuwa ilikuwa siku ya jumapili. nikaendelea na safari yangu ya ukaguzi wa miundombinu itumikayo katika kutoa elimu kwani naamini ili jamii iendelee lazima itumie elimu. Mara nyingi nchi imeingia katika matatizo kutokana na Maamuzi kufanywa kisiasa bila kushirikisha elimu ihusuyo maamuzi hayo. Wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali ni muhimu kushirikishwa katika kufanya maamuzi muhimu katika nchi, wenzetu wa nchi zilizoendelea hawachukui uamuzi bila ya kupitishwa na wasomi wao. Kama wasomi hawatashirikishwa katika maamuzi ya nchi maendeleo yatakuwa ni ya kubahatisha. na Hapo tutajiuliza nini basi maana ya elimu kama haitumiwi itakiwavyo?..

No comments: