Monday 6 August 2007

Hii shule imeahidiwa kujengwa kwa Mawe...


Hicho kibanda unachokiona kwa mbali ni shule huko Mto wa Mbu Arusha, Wafadhili waliahidi kuijenga shule hiyo kwa kutumia mawe badala ya makuti, miti na udongo ili watoto wa maeneo yanayozunguka wapate sehemu bora ya kusoma. sijui mpaka sasa wamefikia wapi lakini jiwe lamsingi lilishawekwa toka mwaka 2000. Natarajia nitakapopita tena nitakuta shule bora iliyojengwa kwa mawe ama matofali na kuezekwa mabati ama vigae. Wenzetu wameendelea baada ya kuipa elimu kipaumbele kama chachu ya kuleta maendeleo, wakaweka mazingira ya kushindana kuvumbua mambo yatakayo rahisisha na kuboresha maisha yao.. haikuwa rahisi lakini kwa kuwa walikuwa na nia, nguvu, dira, na hamasa wamefika na wanazidi kwenda mbele..tujiulize sisi tuko wapi..?

1 comment:

WoodPeckers said...

hongera kwa kuandika habari nzuri na zenye kuelimisha na kuijenga jamii.

Shule sasa imejengwa kwa mawe(matofali)na ina madirisha ya vioo.Kwa kweli inapendeza sana.