Monday, 6 August 2007

Tutaijenga Hosteli Kwa Mikono Yetu Wenyewe....

Nguvu tunazo, mawe tunayo, nia ya kujenga hosteli tunayo tunachohitaji ni msaada tu wa kiufundi. Wanafunzi hawa walishiriki kujenga hosteli ya wasichana shule ya Mukulat Pale Ngaramtoni huko Arusha.
Na madada hawakukaa bali walisaidia mno katika kutafuta mawe kwa ajili ya msingi wa jengo hilo kama wanavyoonekana kwenye picha.

Huyo ni fundi aliyesaidia kuweka sawa msingi wa jengo ili uwe imara, Mtaji wa Masikini ni Nguvu zake na Mtaji wa Shule ni wanafunzi wake...


Matokeo yake...Ni Hosteli ya nguvu iliyojengwa kwa nguvu za wanafunzi, kama kila mwaka shule zingekuwa zina miradi ya kujijengea miundo mbinu kama hii tungefika mbali mno...Hapa cha kujifunza ni kwamba Waafrika Tuamke sio kusubiri misaada(Hand-outs) tunaweza kufanya mambo kwa kutumia malighafi tulizonazo tunachohitaji ni fikra tu jinsi ya kuligeuza jiwe likawa nyumba. Misaada bila fikra tutabaki ombaomba daima..No comments: