Wednesday, 15 August 2007

Hivi Mwalimu Hakujua.....

Kama Tanzania ni nchi yenye Madini, mafuta, gesi, ardhi yenye rutuba, maliasili kwenye mbuga, mbona hakubinafsisha kwa kasi mali hizo wakati alikuwa na nia ya kuinua maisha ya wananchi wake..? Ukiangalia historia yake kuna ukweli tosha kuwa alijua hayo lakini pia alijua dhamira ya hao wawekezaji toka mataifa ya magharibi.. MFUMO WA UCHUMI WA NCHI ZA MAGHARIBI NI UNYONYAJI KWA GHARAMA YEYOTE ILE..

Pia Nafikiri alijua kwa hakika hakuwa na wasomi wa kutosha wa kuweza kusimamia miradi itakayotumia malighafi tulizonazo kwa hiyo kwa busara zake akaweka Kipaumbele kwenye Elimu ili tukishapata wasomi wa kutosha ndipo tuanze kutumia utajiri wetu asilia. Cha Kushangaza leo hii Nchi imesahau umuhimu wa elimu na kuacha watu wakijiita Madokta wakati hata darasani hawajaingia, watu wenye Vyeti feki wakijitamba kuwa sio lazima uwe na elimu kuongoza ama kuleta maendeleo, hawa hawa ndio wanapewa madaraka na kutokana na ukosefu wa elimu wanaingia Mikataba na watu waliobobea katika ku-(manipulate) kutumia ujanja ili kujinufaisha zaidi hali ya kuwa wenye mali wanabaki kuwa waangaliaji tu bila kufaidi mali yao. Nina Uhakika wale waliopokonywa mashirika baada ya uhuru wamerudi kwa kasi kuvuna kilichobakia kwa kasi mpya kabla ya watu hawajastuka. Elima ni kifungua macho na pia inawezesha kuona mbali zaidi ya mlo wa siku moja..

VIONGOZI WANABINAFSISHA MIHIMILI YA UCHUMI WA NCHI KWA AHADI YA MLO WA SIKU MOJA...MAJUMBA MAKUBWA YENYE KWENDA HEWANI, JUMBA LA BUNGE LA GHARAMA SIO KIPIMO CHA MAENDELEO YA NCHI...KAMA MALI YOTE INAMILIKIWA NA WACHACHE WAKISHIRIKIANA NA WAGENI... TULIOBAKI TUFANYE NINI.?..

MISHAHARA DUNI KWA WAFANYAKAZI NI KWASABABU HAKUNA ANAYEJALI KWAKUA PESA ZINAZOPATINA NI ZILE ZITOKAZO NJE na kukandamizwa wafanyabiashara wa ndani. NANI ATAJALI MFANYAKAZI AMEKULA NINI, MZOA TAKA BARABARANI AMESHINDA VIPI, MANESI HOSPITALINI NA WAGONJWA WAKO HALI GANI..

WABUNGE NI WASAHAULIFU TENA WASHABIKI WA VYAMA NA SIO MASLAHI YA WANANCHI WALIOWAWEKA BUNGENI..PENGINE HUONA FAHARI WAKIPITA KWENYE MITAA ILIYOCHOKA NA KUNUKA HUKU WAO WAKILA VIYOYOZI NDANI YA MASHANGINGI YAO TINTED...

MWANANCHI WA KAWAIDA NI SHIDA TU KWENDA MBELE BEI YA KUWASHA KOROBOI IMEPANDA BORA TULE KABLA YA JUA HALIJAZAMA LA SIVYO NI GIZANI MPAKA ASUBUHI..NA HIYO NDIO HALI BAADA YA MIAKA 46 YA UHURU...PENGINE TUKUMBUSHWE SABABU ZA KUGOMBEA UHURU MAANA WENGINE TUMEZISAHAU...

mpaka MLALAHOI atakapojua ATAKULA NINI KESHO KABLA JUA LA LEO HALIJAZAMA hapo ndipo tutakuwa tumepiga hatua....

2 comments:

Anonymous said...

Kweli usemayo viongozi wamepinda

Anonymous said...

Kweli kaka yote usemayo niukweli mtupu.Nami pia natamani sana kama mwalimu angelikuwapo sasa sijui ingekuaje.Yote tisa kilichobaki tupambane na viongozi wote ambao ni wasanini kuanzia Raisi wetu kwani kamaangekuwa sio msanii mafisadi,wauza madawa yakulevya wote wangekamatwa nakufilisiwa.Yeye kakazania kuunda tume kilasiku ya mungu,pesa itumikayo ni yetu wananchi kweli mungu yupo.
Sina mengi ni mimi niombaye kilasiku yamungu tupate viongozi bora na sio bora viongozi.