Monday, 27 August 2007

Urithi wetu Asilia Unavyo Yoyoma

Vitabu vya dini vina himiza waliopewa dhamana ya mali ya watoto yatima kuwa waangalifu na waadilifu tena wasitumie mali kwa kufuja na kujinufaisha wao binafsi. sisi watoto wa watanzania ni sawa na hao yatima na viongozi wetu ndio wenye dhamana ya kututunzia utajiri wa asili tuliojaaliwa na Mwenyezi Mungu ili tuje kunufaika tutakapo kuwa tayari kiuwezo na kielimu kuvuna maliasili zetu ili tuondokane na umasikini huu wa kujitakia. Mimi SI mwanasiasa lakini hupenda kutumia bongo langu kufikiria, hivi kama kweli viongozi wetu wana nia ya kututoa katika umasikini kwa nini isisomeshe wabongo katika fani hii ya uchimbaji madini na kuweza kuunda mashirika ya serikali katika uchimbaji, usafishaji wa madini yetu badala ya kuuza ardhi yenye shehena ya madini kwa wawekezaji ambao wengi wao hawana uchungu na nchi yetu na lengo lao kuu ni kuchukua madini na kujinufaisha na wala sio kutuendeleza na kutusaidia kuondokana na dimbwi hili la umasikini. Kwa hesabu ndogo tu kama matarajio yao ya chini ni kuzalisha 2.6 million Ounces za Dhahabu (hii inatoka kwenye website ya Barrick Gold kwa Mgodi wa Buzwagi), kwa sasa soko la dunia Ounce Moja ya dhahabu ni zaidi ya Dola 600, Piga hesabu mwenyewe wakati wao wametumia millioni 400 USD utakuta ni 1.6 Billion USD ukitoa gharama za kuzalisha Ounce moja ya dhahabu utakuta faida yao ni asilimia 200 za msingi waliotumia hapo huja taja matarajio ya Tani elfu 54 za Copper zilizopo hapo mgodini na hayo NI makisio ya chini. Ukiangalia taathira za uchimbaji huo kwa jamii inayozunguka migodi hiyo ni hakika kuwa mabadiliko ni machache katika uboreshaji wa maisha ya wananchi. Migodi ni sehemu moja tu ya utajiri tuliojaaliwa kuwa nao kuna mbuga ambazo kabla ya wazungu kuja afrika kulikuwa na mamilioni ya wanyama wa aina tofauti lakini leo tumebaki na mamia ya wanyama na kila siku hao waliobaki wanahamishiwa kwenye MA-ZOO nchi za ulaya kwa kisingizio cha kuhifadhiwa dhidi ya majangiri, lakini ukweli ni kwamba itafika siku ukitaka kuona wanyama mwitu itabidi uende Ulaya uone wanyama tena kwa kuwalipa pesa SI BURE. Kutokana na hali ya Usalama kutokuwa ya uhakika katika nchi nyingi za afrika ikiwemo Bongo watalii wengi huenda kuona wanyama kwenye MA-ZOO Ulaya na hata wameanza kujenga mifano ya mbuga za afrika huko AMERIKA tena kwa kufuatilia kila detail ya mbuga kuanzia vichuguu mpaka mito na mabonde mpaka vibanda vya wamasai na wamasai wenyewe kiasi itafika kipindi watu wataenda SERENGETI YA BUSCH-GARDENS iliyoko Marekani kwasababu inawanyama wengi kuliko Serengeti halisi iliyoko afrika. VIONGOZI WETU KUWENI WAADILIFU NA WAONA MBALI, KUUZA MALIASILI KWA BEI YA MLO WA SIKU MOJA INATUANGAMIZA SASA NA HAPO BAADAYE. TUJIFUNZE KUTOKA KATIKA NCHI KAMA DUBAI, MALAYSIA NA KWENGINEKO AMBAKO MIRADI YAO NI KUENDELEZA NCHI NA WANANCHI WAO NA SI VINGINEVYO. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA AFRIKA PIA.

No comments: