Wednesday, 5 September 2007

Kama ningelikuwa ...MWALIMU darasani

Ningefundisha masomo yatakayosaidia kuinua jamii toka kwenye dimbwi la umasikini. ningerekebisha mitaala isiyo na manufaa na wanafunzi, ningependekeza elimu vitendo zaidi ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa wabunifu katika masuala mbalimbali badala ya kuwafundisha kukariri vitabu. ningehakikisha natumia vitabu vya kisasa zaidi ili elimu nitakayotoa iwe inakwenda na wakati. ningewapa wanafunzi uwezo wa kutumia akili zao katika kutafuta majawabu ya matatizo yanayoikabili jamii kila siku na pia kuhakikisha mawazo yao yanafanyiwa kazi kwa vitendo. ningefundisha madhara ya rushwa kwa jamii ili wanafunzi hao waichukie kwa kuwa ndio adui wa maendeleo yao. Elimu tuliyonayo sasa ni ile tuliyoirithi toka kwa WAKOLONI, ambayo lengo lake ilikuwa kuelimisha wachache ili wawe vibaraka na jamii ilobakia iwe ni wenye kuongozwa bila kujua haki zao na wabaki kuwa ni wafanyakazi katika kunyonya mali za nchi yetu kwa manufaa ya WAKOLONI hao. ELIMU ya Mkoloni imejengwa kwa mfumo wa piramidi, pana ukianzia chini na hupungua kuelekea kileleni. WANAFUNZI milioni huandikishwa shule za MSINGI ili wakimaliza wajue KUANDIKA NA KUSOMA tu. wachache hata wakifaulu mitihani ya DARASA LA SABA inabidi wachaguliwe wale wanaoonekana kufaa kuendelea elimu ya sekondari. hapo ni asilimia 10 ya wote waliofanya mitihani ndio wataoendelea na elimu ya SEKONDARI, waliobaki watarudi nyumbani kuwa wakulima, wavuvi, wabeba mizigo, WEZI,na MAJAMBAZI. hao waliobahatika kwenda sekondari watachujwa baada ya mtihani wa FORM FOUR, ambapo pia ni asilimia isiyozidi kumi watakwenda FORM FIVE na SIX, na baada ya hapo wachache watachaguliwa kwenda vyuo vikuu. JAPO TUNAONA MABADILIKO LAKINI HATA MITAALA ITUMIKAYO SASA NI ILE YA WAKOLONI, VITABU VITUMIKAVYO VIMEPITWA NA WAKATI, HAKUNA USIMAMIZI WA KUTOSHA WA KUANGALIA UBORA WA ELIMU TUIPATAYO, WENGI WANAMALIZA FORM SIX NA ENGLISH BADO YA UGOKO. HAO WANAOPELEKWA NJE YA NCHI KUSOMA KOZI MBALIMBALI HAWANA JIPYA WAKIRUDI NYUMBANI KWASABABU MUDA WOTE WAO NI DARASANI, CHUMBANI HAWANA FIKRA ZA KUTOKA NJE YA VYUO KUONA JINSI WENZETU WALIVYOTENGENEZA BARABARA, HOSPITALI, MASHULE, NA MAMBO AMBAYO WANGEWEZA KUJA NA KUIGA ILI KUTULETEA MAENDELEO HAKUNA LABDA WATAKUJA WATULETEE MAMBO YASIO NA MAANA KAMA KUIGA MAMBO YA BIG BROTHER, NA UPUUZI MWENGINE USIO NA MANUFAA KWA JAMII.
ningetumia elimu yangu kubadili mazingira yanayoizunguka jamii yangu na kuweza kutoa chachu itakayoleta mabadiliko katika jamii katika kila nyanja, kama vile kubuni mbinu za kutoa ajira kulingana na mazingira, kuboresha huduma zitolewazo kwa jamii, kuweka wazi mambo na kutumia elimu katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya jamii. je wewe ungefanyaje?

No comments: