Wednesday, 28 May 2008

Vitambulisho Vya nini?


Vitambulisho vya nini katika nchi ambayo hata umeme wa uhakika bado ni changamoto. Mabilioni ya pesa ambayo yangeweza kuhakikisha shule zina vitabu vya kutosha, hospitali zina dawa za kutosha, barabara zinapitika japo kwa msimu wa kiangazi, watu wanaajira japo za kuhakikisha mlo mmoja kwa siku. Vitambulisho vya nini wakati passport zinatosha kumtambulisha mwananchi, vitambulisho vya nini wakati gharama za utengezaji ni kubwa kuliko kipato cha mlengwa. gharama za utunzaji wa kitambulisho hicho ni nani atakayelipa maana kama ni kitambulisho kilichotengezwa kwa kutumia plastiki kina "finite life time", nani atakayelipa "replacement" ya kitambulisho hicho. na kama kitakuwa na "Chip", je vifaa vya kusomea habari zilizopo kwenye hiyo chip vitawekwa kila ofisi iwe ya serikali na binafsi. kwa ufahamu wangu inabidi uwe na central database system ambayo itashughulikia uhifadhi wa habari za mwenye kitambulisho, mambo yanayohitaji kuwa na ma "computer servers " kubwa na pia watu wa kuendesha computer hizo na pia umeme wa uhakika na sio wa mgao si kwenye hizo computer farms bali na hizo "service points". faida za mradi huu kwa hakika zinashindwa na hasara zitakazopatikana, na si baada ya muda mrefu mradi utakufa na mabilioni yaliyotumika yatakuwa ni kama maji yaliyomwagika mchangani. hizo pesa zingetumika katika kutatua matatizo yanayomgusa mtanzania kila siku kama vile upatikanaji wa maji safi "on demand", upatikanaji wa huduma bora za afya na gharama nafuu, upatikanaji wa elimu bora yenye kwenda na wakati kwa gharama nafuu... VIONGOZI WETU WALIOPEWA MADARAKA YA KUFANYA MAAMUZI KWA MANUFAA YA TAIFA WANAFANYA MAAMUZI KWA MANUFAA YA KWAO WENYEWE..TATIZO TULILONALO WAAFRIKA SIO UMASIKINI WA PESA, BALI UMASIKINI WA FIKRA NA ELIMU NDIO UNAOTUANGAMIZA ZAIDI...

1 comment:

markus mpangala said...

Mdogo wangu umenikuna sana na machungu ya nchi hii. ujue kuna watu wameamua kutumaliza kwa madhumuni yao. sijui wanataka ili tuweje. Lakini acha wafanye lakini TIME WILL TELL, TUNASONGA KWA MWENDO WA KARATASI AMA KINYONGA TUNAWAFUATA HUKOHUKO WALIKO SIY HABARI ZA KUWANGOJA CHINI.
keep it up kumbuka kuweka blogu ya jikomboe ya ndugu ndesanjo(www.jikomboe.com) usiandike neno blogspot katika blogu hiyo usije ukaoikosa.
nitembelee www.lundunyasa.blogspot.com.
masomo mema