Friday, 5 June 2009

Bongo hakuna wasomi



Bongo hakuna wasomi kama tafsiri yangu ya usomi ni mtu mwenye kuona tatizo akalitatua kwa kutumia elimu iliyojaribiwa (tried and tested). Msinishambulie kwasababu kama kungekuwa na wasomi tusingekuwa na shida ya maji wakati maji kila siku yanatiririka kwenye mito kuelekea baharini bila ya kupingwa.


Kungekuwa na wasomi wangejenga mazuio ya maji yasiende baharini ili yatumike kwa shughuli mbalimbali. na tusingepanga foleni zenye urefu wa maili kusubiri zamu ya kukinga dumu ili upate maji ya kunywa.


kama kungekuwa na wasomi barabara zetu zingetosha na foleni ya magari isingetungiwa nyimbo. na watu wasingetoa wazo la kugawa barabara moja njia tatu. mipango miji ingekuwa wazi na mamlaka husika wasingekuwa wakipata gharama za kuvunja nyumba za masikini na masikini kupata machungu zaidi maana kubomoa ni siku moja lakini kujenga ni kazi ya miaka.


kungekuwa na wasomi elimu ingekuwa ya manufaa na maisha ya wananchi yangeinuka na kupanda kiwango kila mwaka.


kungekuwa na wasomi huduma za afya zingetolewa bila rushwa na pia zingekuwa za uhakika wagonjwa wa miguu wasingepasuliwa vichwa na wagonjwa wa vichwa wasingepasuliwa miguu. ingekuwa ukifika hospitali una mategemeo ya kupona na si kumalizwa kabisa. wagonjwa wasingelazwa sakafuni, wagonjwa watatu wasingelazwa kitanda kimoja. na wodi za wagonjwa zingekuwa safi kuepusha maambukizi ya magonjwa.


kungekuwa na wasomi viwanja vya wazi visingemilikishwa kwa watu na badala yake kungekuwa na bustani na viwanja vya michezo mbalimbali. nyumba zingejengwa kiholela na kutengeza mijiovyo (slums) badala ya mipango miji safi.


kungekuwa na wasomi nisingeandika mada hii.....

1 comment:

Anonymous said...

I LIKE THIS MY SON. ILI NCHI IENDELEE INAHITAJI VITU GANI(AS PER MWALIMU JKN)NADHANI VYOTE TUMEFAULU KASORO KIMOJA SIASA SAFI.
SIASA IKIWA MBOVU KILA KITU KINAKUWA OVYO, WATU WATAKUWA WAKIJIPENDA WENYEWE KULIKO KUPENDA NCHI YAO.