Thursday, 26 July 2007

Fundi Mchundo Toka USA

Huyu ni mmoja wa Mavolunteer toka USA waliofika Arusha na kuanza kukarabati baadhi ya majengo mabovu ya shule. Hivi wewe uliye Majuu unaweza kurudi bongo wakati wa holiday na kushika karai na mwiko kuanza kukarabati shule ya msingi uliosomea mpaka leo ukafika huko uliko?.
Kujitolea muhimu ndio maana wenzetu wapo walipo sasa kwasababu babu zao, bibi zao walijitolea kujenga majumba, mashule, mahospitali na hata mabarabara. Hivi kama wao Wameweza tujiulize wana NINI ambacho sisi hatuna mpaka sie tushindwe kufanya mazuri wanayofanya wao?

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Kazi Nzuri !

Ibrahim said...

Keep The good work , Young boy!