Friday 27 July 2007

Umuhimu wa Maji-Korogwe

Wanafunzi wa Sekondari ya Korogwe wakifurahia upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali tofauti na wanafunzi walioko Pugu Dar es salaam wanaohangaika kutafuta maji kutwa ama kununu dumu moja sh 800 bila kujua maji hayo kama ni safi ama machafu. Tumezungukwa na Maziwa makubwa yenye maji baridi kama vile Ziwa Tanganyika lenye kubeba 1/6 ya maji baridi yote yaliyopo duniani lakini mpaka leo wananchi wanaozunguka ziwa hilo wanaukosefu wa maji kwenye mabomba yao. Tuna mito itiririshayo maji baharini mamilioni ya lita kila siku lakini maji ya kuoshea vyombo ni tabu kupatikana. Tujiulize hivi shida hizi zitaisha lini, nafikiri ni wakati wa kutumia akili, maarifa, kutafuta wataalamu wenye fikra za kuendeleza nchi ili tupate kujitoa katika matatizo kama haya tusisubiri wafadhili waje kutuletea maji ya kunywa. Wadau Changieni Hoja ili tuamshe akili na maarifa...katika kuleta mabadiliko.. Nchi yetu inauwezo wa kuwa kama nchi zilizoko Ulaya kama tutaamua kuendeleza rasilimali na maliasili zilizopo.

No comments: