Friday, 27 July 2007

Jifunze Kujitwika Maji Kwa Ngata

Hawa ni Volunteer waliojitolea kuja Tanzania kwa ajili ya Kuchimba visima kwa ajili ya matumizi mbalimbali wakijifunza kujitwika ndoo ya maji kwa kutumia Kanga. Ni mtihani mzito kwa waliozoea kufungulia maji ukiwa ndani ya nyumba. Hakuna maneno yatakayotosheleza kuelezea umuhimu wa upatikanaji maji. kwa ufupi bila maji hakuna kiumbe kitakachoishi iwe miti, wadudu, wanyama na pia ardhi hufa kama hakuna maji. Maji ndio maisha na ukiweka mbele umuhimu wa upatikanaji maji basi kila kitu kitakaa sawa iwe mashamba, nyumba, vijiji, miji na nchi kwa ujumla. Siku nyengine tunaenda shule bila kuoga kisa maji hakuna. sasa unafikiri harufu ya jasho ya darasa zima kuna somo litakalopanda hapo.. Uwezekano wa kuwa na maji upo kwanini mambo yawe yamekauka wiki nzima..Tuma wazo..

No comments: