Friday, 27 July 2007

Visiwa Vya Peponi...Paradise Island

Hiyo ni sehemu ya Kisiwa Cha Chumbe kilichopo Zanzibar, Tumejaaliwa pepo lakini tunaona tuko Motoni. Hebu Tazama uzuri wa madhari ya kisiwa hichi, ni watalii tu ndio wenye macho ya kuona vizuri, nahisi macho yetu yana vumbi tena vumbi la fikra. Utalii sio tu wazungu toka Ulaya, hata sisi wakutoka uswahilini tunaweza kwenda kutembea kujionea wenyewe uzuri wa nchi yetu. Utalii wa ndani inabidi upewe kipaumbele kwasababu utaibua akili z kuhifadhi mazingira hivyo kuendelea kufaidi hewa safi, pwani safi, hata viumbe viishivyo baharini vitaongezeka na kufaidisha wavuvi na watu wote kwa ujumla. UKIPENDA MAZINGIRA NAYO YATAKUPENDA.. au Unabisha? toa hoja

No comments: