Thursday, 26 July 2007

Ndege Huyu Ndege Gani?

Rangi yake ya Kupendeza Machoni, Sauti yake Haichoshi Masikioni, Mruko wake ni maridadi angani, lakini ndege huyu ndege gani? Tumejaaliwa Wanyama, ndege, wadudu wa kila aina wengine hupatikana hapa kwetu tu, Wenzetu wanathamini wanyama kiasi kuwezi kwenda porini kuangalia ndege aina fulani bila ya kibali maalum. sisi ukimuona mwewe tafuta jiwe umpige! Imefika wakati nasi tuanze kuthaminisha maliasili tulionayo na sio kuiuza kiholela kwa pesa ya kula siku moja. ndege, wanyama kibao husafirishwa kwenda kwenye ma zoo ulaya, siku itafika ukitaka kuona simba itabidi wende ulaya maana wote tushawauza.

No comments: