Thursday, 16 August 2007

Uwekezaji au Uchukuaji...


Kuwekeza kwa maoni yangu kuwe na manufaa na mahala panapoekezwa iwe ni mgodi, kiwanda, nyumba ama kitu chochote kitakacholeta manufaa kwa wanaouzunguka hicho kilichoekezwa, kwa mfano kila unapochimba mgodi kuna matokeo mawili, la kwanza ni kupatikana kwa kile unachokichimba na pili ni uharibifu wa mazingira ya hapo ulipochimba. kama ujuavyo kila mchimbaji huacha shimo kama kilichochimbwa hakitarejeshwa mahala kilipokuwa. Uharibifu wa mazingira katika migodi ni wa kudumu kwa hiyo lazima fikra za kuweza kujaribu kuziba uharibifu huo lazima upewe kipaumbele kama jamii izungukayo migodi hiyo iweze kuendelea kwa kutengenezewa vipato mbadala ili mgodi unapokufa pawe na njia nyengine ya kupatia ajira hao wafanyakazi na pia hao wanaozunguka mahali hapo. kama dhahabu, almasi na madini yote yatakwenda kusafishwa nje nchi pesa ambayo ingepatikana katika shughuli za usafishaji huo hazitopatikana na badala yake itakuwa ni uchukuaji na si uwekezaji tena. na matokeo ya uchukuaji ni kuachwa kwa mashimo matupu ardhini ambayo ni hatari kwa mazingira ya mahala hapo. Kama kweli ni wawekezaji basi waje na kitu kamili, wajenge mitambo ya kusafisha, wajenge maduka ya kuundia vito hapo hapo penye kuchimbwa madini hayo na sio kuyachota na kuyapeleka kwao na kuyapa faida zaidi(value added) wakishayaunda kuwa vito vya thamani ama kwa matumizi mengine. wakijenga mitambo itakuwa ni ajira kwa wazawa, wakijenga maduka tutapata ajira na miji itakuwa kutokana na faida ya wanunuzi toka nje wakinunua kitu kilichoongezewa thamani na hivyo kulipa taifa faida zaidi na kuinua hali za maisha za wananchi wake tofauti na ilivyo sasa. tujiulize kwanini dhahabu ichimbwe afrika ikasafishwe ulaya...sie tuuze bei ya mchanga wao wakauze dhahabu huu ni ujinga wa hali ya juu, bora ibaki ardhini mpaka tutakapo kuwa tayari kuichimba wenyewe kuliko kuibiwa hali tuko macho...

No comments: