Thursday 20 September 2007

Elimu na Mitihani.....

Mitihani ni kipimo cha maendeleo ya mwanafunzi katika masomo anayofundishwa, Mfumo tulionao ili uweze kwenda mbele lazima ufaulu mtihani wako wa mwisho katika kila daraja la elimu iwe darasa la saba, form four, form six ama hata mitihani ya mwisho wa semester chuo kikuu. Mara nyingi imejitokeza hali ambayo mitihani huibiwa kabla na kuuzwa kwa watoto wenye pesa ili waweze kukariri majibu na kuweza kufaulu kirahisi, hata imebainika kuwa baadhi ya shule kutumia wanafunzi waliokwisha maliza kufanya mitihani kwa ajili ya watoto wengine. hali hii iko katika ngazi zote za elimu..kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. matokeo yake ni kupata viongozi wabovu wasio na elimu ya kutosha ya kuweza kufanya maamuzi yatakayoleta maendeleo ya nchi. Japo juhudi za ujenzi wa sekondari kila kata ama wilaya utapelekea kuwa na shule za kutosha kukidhi mahitaji ya wanafunzi lakini kama hakuna vifaa vya kutosha katika shule hizo ama hakuna walimu wenye sifa za kutosha katika shule hizo, taifa litapata hasara ya kukosa Nguvu kazi stadi. Ubora wa elimu uzingatie mahitaji ya jamii.. jamii kwa sasa inahitaji madaktari, manesi, mafundi bomba, mafundi umeme, mafundi nyumba, na pia seremala, watengeza magari na pia watengeza vitu vya eletroniki. kama elimu itaanza kulenga mahitaji ya jamii na nchi kwa ujumla itaibua ajira na hivyo kuboresha maisha ya watu wake. KUIBA MITIHANI hakutaisaidia nchi bali kuiangamiza. PIA MITIHANI ISIWE KIPIMO CHA MWISHO CHA UWEZO WA WANAFUNZI, MAENDELEO YAO SHULENI KWA UJUMLA NDIO IWE KIPIMO , MARA NYENGINE UNAWEZA KUWA NA UFAHAMU MZURI WA MASOMO LAKINI KUTOKANA NA HALI INAYOWEZA KUJITOKEZA SIKU YA MTIHANI UKASHINDWA KUFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI HUO...

1 comment:

Anonymous said...

vizuri kuanza